Meya wa Jiji la Dare s Salaam, Omary Kumbilamoto.
BAADA ya kumfichaficha kwa muda mrefu, hatimaye mume wa mtangazaji Khadija Shaibu ‘Dida’ amejulikana ambaye ni Meya wa Jiji la Dare s Salaam, Omary Kumbilamoto.
Video mbalimbali zilizovuja usiku wa jana baada ya Dida kufunga ndoa, zilimuonesha Dida akiwa amevalia shela la harusi akiwa kwenye hoteli ya Serena peke yake bila ya mumewe.
Mapema leo hii ndipo imefahamika kuwa Dida kaolewa na meya huyo na kwamba sherehe za wawili hao bado zinaendelea kwa siku tatu mfululizo.
Hii ni ndoa ya nne kwa mtangazaji huyo. Dida aliwahi kuolewa na Juma Mchopanga ‘Mchops’, Gervas Mbwiga ‘G’ kabla ya kuolewa na mtangazaji mwenzake, Ezden Jumanne Ntambi na wote hao ameshatemana nao.
Stori: Sifael Paul