Haya ndo maajabu ya mti wa Mlonge

 


Mlonge ni mti maarufu sana Duniani kote hata hapa Tanzania hususani Mkoa wa Kigoma, Kila sehemu ya mti wa mlonge hutumika kwa dawa. Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga pia hata mbegu zake zinafaida mwilini kutibu baadhi ya magonjwa.


Baadhi ya faida zitokananzo na Mti wa Mlonge ni pamoja na kutibu maradhi mbalimbali kama  Pressure, malaria,  homa ya mara  kwa mara,saratani ya tumbo, hupunguza sonona , huleta hamu ya kunywa maji, jambo ambalo ni adimu   kwa watu wengi pia huondoa uchovu mwili na kukufanya uwe na afya nzuri, lakini pia matumizi ya mlonge husaidia kurekebisha viwango ya sukari katika mwili wa mwanadamu.


Majani na maua ya Mlonge  yanavirutubisho vingi kama vitamin A mara tatu zaidi ya karoti), Vitamini C mara tatu zaidi ya ile ya machungwa, calcium mara 140 zaidi ya ile  inayopatikana katika maziwa ya ng’ombe na Potasiamu.


 Mmea huu umetumika kusadia   udhibiti wa matatanisho yanayoletwa na ugonjwa wa ukimwi, pia unga wa majani ya mlonge yanaweza kutumika kama mbadala wa dawa za kutibu maji kama vile waterguard.


Aidha  Kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini ya chuma (Iron), kasiamu (Calcium) na vitamin   nyingi za aina  mbalimbali, majani ya mmea huu yamekuwa yakitumika kama ‘tonic’ kwa   watoto wadogo na vijana ili   kuimarisha mifupa na kusafisha mfumo wa damu mwilini.


Faida nyingine Majani yake huweza kupakwa mwilini katika kutibu majipu na maambukizi ya ngozi na  kutumia majani ya mlonge kama unavyotumia mchaichai na hapo unakuwa unaibu ugonjwa wa Malaria.


Mmea wa Mlonge ndio mmea ulio na kiwango kikubwa cha virutubisho vyenye manufaa kwa  mwili wa binadamu na mifugo. Una virutubisho zaidi ya 90 na unaweza kutumiwa na watu wa  umri wote Hakuna Madhara yoyote ya kutumia Mlonge ambayo yamethibitishwa na wataalamua.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad