Hofu yakumba kijiji cha Afrika Kusini kinachodaiwa kuwa na almasi




Kundi kubwa la watu limekusanyika katika kijiji kimoja mkoani KwaZulu-Natal ambako kumetokea uvumi wa kupatikana kwa madini ya almasi, kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini Afrika Kusini.
Video zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha watu wakichimba ardhi kutafuta mawe hiyo ya thamani .

Mamlaka ya mkoa pia imeweka kwenye Twitter kanda ya video ikielezea wasiwasi wake kuhusu "watu wanakimbilia almasi".

iliongeza kuwa "imepokea kwa wasiwasi, ripoti za shughuli za uchimbaji haramu zinazofanyika KwaHlathi nje kidogo ya mji wa Ladysmith".

Mamlaka za mitaa bado hazijathibitisha ikiwa mawe hayo ni almasi halisi.

Idara ya kitaifa ya madini na nishati inasemekana imeahidi kutuma timu yake - pamoja na vitengo vya utekelezaji na uzingatiaji, pamoja na wanasayansi wa jiolojia - kukagua eneo hilo.

Utawala wa KwaZulu-Natal pia umesema katika taarifa ya vyombo vya habari kwamba unahofia msongamano wa watu unaweza kuchangia ukiukwaji wa kanuni za kudhibiti maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Covid-19.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad