Idadi ya Wagonjwa wapya wa COVID-19 Nchini Uganda imefikia Watu 1,000 kwa siku hali ambayo imeleta hofu na mashaka kufuatia kufurika kwa Wagonjwa mahututi Hospitalini na kufanya mfumo wa afya kuzidiwa huku msongamano wa magari ya kubeba Wagonjwa kwenye Hospitali kuu ya Mulago.
Inaelezwa kwamba hii imetokana na idadi kubwa ya Watu kupuuza kanuni za kudhibiti ugonjwa huo hata baada ya aina za virusi kutoka Uingereza, Afrika Kusini, India na Nigeria kugunduliwa.
Rais Museveni na Mkewe walipata chanjo yao ya pili na kuwahimiza Raia kwenda kupata chanjo hiyo ya bure ambapo japo wengi wameitikia wito huo lakini wengine wana mashaka kuhusu usalama wa chanjo hiyo.