Irene Uwoya "Wabongo punguzeni roho mbaya, mtu akikuzidi kubali"




Staa wa filamu nchini Irene Uwoya amerusha jiwe gizani baada ya kupost picha yake kwenye ukurasa wake wa Instagram kusema wabongo wapunguze roho mbaya kwani haitawasaidia kitu.
Ujumbe huo wa Irene Uwoya ameutoa kupitia akaunti yake ya instagram na kusema kuwa;

"Wabongo punguzeni roho mbaya haitawasaidia kitu, mtu akikuzidi kubali huyu kanizidi acha kutafuta kasoro hazina kichwa wala miguuu, wengi wenu mnashindwa kufanikiwa sababu mpo busy kushusha wenzenu na kuwatafutia kasoro badala ya kujiombea mambo yako yaende"

"Baraka zako zipo kwa watu wanavyokuombea sasa wewe toka uzaliwe huna zuri unawazia wenzako vibaya una tafuta kasoro za watu huwezi kufanikiwa maisha, huo muda unaotumia kuchukia watu embu muombe Mungu abadilishe maisha yako"

"Utabaki unalalamika tu Mungu nimekosea wapi kumbe roho yako mbaya ndio inakuponza, jifunze kwa walio kuzidi acha chuki za kijinga hazitakusaidia unapoteza muda na baraka zako" ameandika Irene Uwoya

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad