Jeshi la polisi lamshikilia House boy anaedaiwa kuua Mama na watoto wake

 


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia Shadrack Kapanga mwenye miaka  (34), Msaidizi wa kazi za ndani (House boy) kwa kosa la kuwauwa wanafamilia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro amesema June 11, 2021 majira ya 17:00hrs walimkamata mtuhumiwa Kapanga kwa tuhuma hizo. 


Wanafamilia hao waliouawa ni EMILLY MUTABOYERWA (Mama) na wanae DANIELA MUTABOYERWA (15) na DAMITA MUTABOYERWA (13) huko maeneo ya Masaki mtaa wa Maryknol nyumba Na.1224 wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad