Rais wa Somalia Mohammed Farmaajo ( kushoto) na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wamekuwa wakikutana mara kwa mara kutanzua mizozo ambayo imekuwa ikiibuka baina ya nchi zaoImage caption: Rais wa Somalia Mohammed Farmaajo ( kushoto) na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wamekuwa wakikutana mara kwa mara kutanzua mizozo ambayo imekuwa ikiibuka baina ya nchi zao
Kenya imeonya kuwa inaweza kuweka marufuku kabisa kwa ndege kutoka Somalia pamoja na zile za misaada ya kibinadamu.
Wizara ya maswala ya kigeni ilisema katika barua kwa ujumbe wa kidiplomasia kwamba safari za misaada ya kibinadamu zinatumiwa vibaya kwa "mambo ya nchi hizo mbili na kisiasa" hata baada ya Kenya kusitisha safari zake.
Hivi majuzi Kenya ilisitisha safari za ndege kutoka nchi hiyo jirani lakini ilisamehe safari za dharura za matibabu na zile zilizo kwenye shughuli za misaada ya kibinadamu za UN.
Lakini sasa inaonya kuwa "safari za kibinadamu lazima zitumike kabisa kwa madhumuni ya kibinadamu ili kuepuka tangazo linalowezekana na serikali ya Kenya la kuzuiliwa kabisa kwa ndege zote".
Wizara pia imehitaji ndege zote za misaada ya kibinadamu kutafuta kibali kwanza - na kutoa orodha ya abiria pamoja na bidhaa zinazosafirishwa.
Kenya na Somalia zimekuwa katika mzozo wa kidiplomasia kwa muda mrefu, pamoja na mzozo wa mpaka wa baharini ambao umeendelea tangu 2014, wakati Mogadishu ilipoleta kesi dhidi ya Kenya katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki.
Awali Somalia ilikata uhusiano wa kidiplomasia na Kenya mnamo Desemba, ikiishtumu kwa kuingilia masuala yake ya kisiasa ya ndani - kwa kuunga mkono utawala wa eneo lenye uhuru la Jubaland
Mnamo Mei 6, ilisema kwamba uhusiano wa kidiplomasia umerejeshwa baada ya upatanishi wa Qatar lakini Kenya ilisitisha safari za ndege wiki kadhaa baadaye. Kenya inasema kwamba anga yake na Somalia bado imefungwa kwa sababu ya kukatika kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.