Msanii wa Konde Gang Official Killy, amesema hajawahi kuwasiliana na Alikiba tangu ahame lebo ya Kings Music Record ila kwa mara ya kwanza walikutana kwenye msiba na wakasalimiana fresh kabisa na hana noma naye.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television.
"Sijawahi kuwasiliana naye lakini kuna mahali tumeshawahi kukutana tukasilimiana, akatuambia wadogo zangu vipi mpo poa ilikuwa kwenye msiba, hana noma kwa sababu hatukuwa na matatizo na tuliondoka pale kwa amani na tulimuaga, pia sijamu-unfollow kwenye Instagram" ameeleza Killy
Killy na Cheed walihama lebo ya Kings Music Records ya Alikiba mwezi Aprili 2020 na kusainiwa lebo ya Konde Gang Music Worldwide ya Harmonize.