Kitambulisho Cha NIDA Sio Kigezo Cha Kutokuulizwa Uraia Wako

 


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene amesema kupewa kitambulisho cha NIDA sio kwamba huwezi ukaulizwa uhalisia na uhalali wa uraia wako


Waziri Simbachawene amesema hayo Bungeni leo Wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Kirumbe Ng'enda lililohoji "Ni lini serikali itakamilisha zoezi la utoaji wa vitambulisho vya NIDA kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma ili waondokane na usumbufu mkubwa unaotokana na doria za uhamiaji Mkoani humo."


"Kupewa kitambulisho cha NIDA cha uraia wa Tanzania sio mwarobaini kwamba wewe sasa huwezi ukaulizwa uhalisia na uhalali wa uraia wako, hata wakazi wasio raia wanapewa vitambulisho hivi kwani kuna madaraja tofauti tofauti ya upewaji wa vitambulisho,"


"Sio kwamba ukipewa kitambulisho hiki hutaulizwa tena, hata mimi naweza nikaulizwa uraia wangu hata kama nina kitambulisho endapo hata natoka Dodoma nitaulizwa kitambulisho, nitaulizwa uraia na uhalisia endapo kutajitokeza wasiwasi wowote

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad