Kwanini Zari tu Ndio Apigwe Mawe Sakata la Ubalozi wa Hiari? Watanzania Tumebweteka


Binafsi kwanza niseme naamini kwenye swala la uzalendo Ila kuamini kwenye uzalendo sio kigezo cha kusema mtu mwingine anyimwe fursa kama nafasi ipo kwa wenyeji na wageni kupata fursa husika.

Nakumbuka siku za hivi karibuni mwanadada @shomadjozi kutoka nchini South Africa aliweza kupewa nafasi ya kuwa BALOZI WA UTALII NCHINI TANZANIA kwa lengo la kwenda kutangaza mema ya nchi yetu.

Kama haitoshi pia mchezaji ambaye anacheza EPL na rais wa Ufaransa @mamadousakho aliweza kutembelea Tanzania na alialikwa bungeni naye akapewa nafasi ya kuwa balozi wa utalii hapa Tanzania na nafasi ikiwa special pia kwake ili aweze kutangaza mema ya nchi yetu.

Hawa wote sikuona malalamiko Wala kelele zozote watu waliona na wakaona Jambo jema wakafurahi.

Leo najiuliza kwanini shida inakuja kwa zarithebosslady kwaninii ???

Yaaani kuona watu wanaigeuza kama kampeni tena kwa "UBALOZI WA HIARI" unaweza kushangaa Hawa watu wanatumia vigezo gani kulalamika au ni mioyo imebeba chuki ambazo zinawafanya wanashindwa kujizuia hata ambayo hayahitaji mjadala wajadili.

Kwanza sidhani Kama ni kweli eti wasanii wa ndani wananyimwa fursa ya kuwa "MABALOZI WA HIARI" kwa sababu mwisho wa siku hilo ni Jambo la kujitolea ningesikia kuna msanii kaandika proposal yake na idea yake ya kutangaza utalii Ila ikakataliwa hapo ningeona malalamiko yana mantiki.

Halafu tukubali tukatae Kuna vitu vinahitaji influence sasa Kama mtu huna ushawishi mkubwa upewe fursa tu kirahisi.

Nani anakataa kwamba zarithebosslady sio mwanamke mwenye influence kubwa zaidi Africa Mashariki,Ila achana na hiyo zarithebosslady yuko connected zaidi na Tanzania pia kwa sababu ana watoto na msanii mwenye influence kubwa saaana pia @diamondplatnumz lakini Kama haitoshi Wana watoto ambao Wana influence ya maana Sana @princenillan na @princess_tiffah je kwa uhalisia huu unakataa kwamba hana uwezo wa kushawishi upande wa utalii Tanzania.

WIZARA YA MALI ASILI NA UTALII wao wamemuona zarithebosslady Kama fursa kuendana na influence yake na wameona kwa strategy zao anafaa kama ambavyo wamefanya kwa @shomadjozi na @mamadousakho

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad