LENGAI ole Sabaya, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, ameachia “waraka mzito,” ukilenga mustakabali wa maisha yake, baada ya kifo cha Rais John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na Sabaya zinasema, waraka huo, aliuachia siku mbili tokea kufariki dunia kwa Dk. Magufuli aliyekuwa rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dk. Magufuli alifariki dunia, saa 12:00 jionitarehe 17 Machi 2021, katika hospitali ya Mzena, mkoani Dar es Salaam. Alizikwa 26 Machi 2021, nyumbani kwao Chato, mkoani Geita.
Sabaya amesema, usiku wa tarehe 17 Machi, ulikuwa ni usiku mgumu mno kuwahi kumtokea katika maisha yake, na kwamba anaisikitikia siku hiyo kwa kuwa amempoteza mtu mwenye upendo ana “anayehukumu baada ya kusikiliza.”
Anaongeza, “…nimempoteza Baba, Mwalimu na mtu mwenye huruma, ambaye kabla ya ‘kukuhukumu’ atataka na wewe akusikilize na siku zote akisema usiogope. Mtu asiyejua unafiki wa kupikwa.”
Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema, pamoja na kwamba waraka wa Sabaya kwa Dk. Magufuli, uliandikwa kabla ya mwanasiasa huyo hajaingia matatani, lakini ujumbe uliyomo kwenye waraka huo, unaweza kuwa na uhusiano mkubwa na pengine wa moja kwa moja na matatizo anayopitia sasa.
Undani wa waraka huo na uchambuzi wa kina wa alichokisema Sabaya ambaye sasa yuko gerezani, soma Gazeti la Raia Mwema, la leo Jum