Wakati toleo jipya la simu za iPhone 12 likizidi kusambaa kwa kasi duniani kote, madaktari wameonya kwamba simu hizo zinatoa mionzi mikali ambayo ni hatari kwa watu waliopandikizwa vifaa vya kuusaidia moyo kwa watu wenye matatizo sugu ya moyo, vikiwemo vifaa vya pacemaker na cardioverter-defibrillators (ICDs).
Taarifa hiyo ya madaktari, inaeleza kwamba wagonjwa wa moyo waliopandikizwa vifaa hivyo, hawapaswi kuweka simu hizo karibu na moyo kwa sababu mionzi hiyo, inaweza kusababisha vifaa hivyo vikazima.
Wanashauri kwamba, simu za aina hiyo, hazipaswi kuwekwa kwenye mfuko wa shati, sidiria, mabegi ya mgongoni au mifuko mingine iliyopo karibu na moyo na kwamba onyo hilo linahusisha pia vifaa vingine kama iPods.
Ripoti hiyo ya madaktari, huenda ikaathiri mauzo ya matoleo mapya ya iPhone12 series duniani kote.