Hii posti ni kwa watanzania wenzangu mnaoishi marekani mliochukua hii PPP loan iliyotolewa kwa ajili ya kusaidia makampuni ili yaweze kulipa wafanyakazi kipindi cha Covid-19.
Kuna Mtanzania mmoja amekamatwa toka majuzi sababu ya hii PPP na alipewa dola elfu 20 tu. Huyu akitoka ndani ni safari ya Tanzania moja kwa moja.
Nimeingia kwenye hiyo website nimeona majina ya watanzania wengi au majina ya kampuni uchwara zao wamepiga hiyo PPP loan. Nimesikitika sana maana wataishia pabaya. Guys there’s no free money in this world.
Angalieni screenshot ya pili kuna Mtanzania anaishi hapa Santa Monica alitaka kunisaidia na mimi nipige dola elfu 20 mara 2, kwa maana hiyo ningepata dola elfu 40 ila nilimkimbiza fastaaaa. Staki kabisa hayo mambo ya u-criminal in my life. 40,000 is not worth mimi kurudishwa Tanzania kama mwizi na kupoteza watoto wangu. Alafu sasa wala asingenipa zote hizo elfu 40, na yeye angekata chake cha juuu.
Tatizo watanzania utapeli hatuujui vizuri hatuna akili. Kuna mkenya kapiga PPP ya karibia dola milioni 3, kabeba pesa karudi zake Kenya fastaaa watamkamatia wapi? Na wanaigeria wamefanya hivyo pia Ila watz mmechukua hela za watu na huku hakuna wafanyakazi mnaowalipa alafu bado mko hapa hapa marekani na vihela vyenyewe mlivyopiga ni vidogo not even worth risking your freedom over na hakuna cha maana mnafanyia hizo pesa zaidi ya kula bata. Watanzania utapeli tuwaachie wanaigeria jamani. Mtakamatwa wooote huko mbeleni. Wamarekani wenyewe wenye nchi yao wanakamatwa kwa ajili ya hii PPP loan ndo sembuse nyinyi wahamiaji?
Alafu this is a federal crime aiseee.