Mariah Carey akanusha kupigana na Jay Z





Mwimbaji Mariah Carey amekanusha uvumi wa kupigana na mmiliki wa lebo ya Roc Nation, Jay Z kama ambavyo mitandao mbalimbali ilivyoripoti taarifa hiyo ikidaiwa kuwa tukio hilo lilitokea mara ya baada ya kikao chao kwenda tofauti mezani.
Mariah Carey kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kwamba, taarifa hizo hazina ukweli. Jay Z na Mariah walishirikiana kuupika wimbo namba 1 duniani #HeartBreaker mwaka 1999.

Aidha,Mariah Carey hayupo tena chini ya usimamizi wa lebo ya Jay Z, Roc Nation baada ya kuachana nao, amesaini mkataba na lebo ya Range Media Partners ambayo itakuwa ikisimamia kazi zake kuanzia sasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad