Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, ametaka suala la kulipa kodi kwenye majengo kuangaliwa vizuri akisema, "Mkaliangalie vizuri huko mtaani. Tusidanganyane, kuna mkanganyiko!"
Ameshauri jambo hilo kuwekwa vizuri kwa Wananchi na kueleweka anayelipa Kodi hiyo ni nani kati ya mwenye nyumba na mpangaji badala ya kusema ulipaji umekuwa rahisi