Mbunge Apongezwa kwa Kutopiga Sakarasi Bungeni




Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mh. Godfrey Kasekenya, na kulia ni Mbunge wa Mbulu vijijini Flatei Massay.

 

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi  Godfrey Kasekenya, amempongeza Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay, kwa kutopiga sarakasi Bungeni, baada ya serikali kutangaza kuanza ujenzi wa barabara inayotoka Mbulu, Haidom hadi Singida kwa kiwango cha lami.

 

Kasekenya ametoa kauli hiyo leo Juni 21, 2021, Bungeni Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu, ambapo amesema kwamba kipande cha barabara cha kutoka Mbulu hadi Haidom kimetangazwa kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa ujenzi wa kipande cha barabara hiyo.

 

“Mheshimiwa Naibu Spika nimshukuru sana leo Massay, hajataka kuruka sarakasi, kama alivyoahidi Mh. Waziri kama hizi barabara zitatangazwa ni kweli zimetangazwa na Km 25 zinaanza kujengwa kwa maana ya bajeti ya mwaka huu na bajeti itakayoanza Julai kuna fedha zimetengwa,” ameeleza Naibu Waziri Kaserkernya.

 

Hivi karibuni Mbunge huyo alitishia kupiga sarakasi Bungeni wakati akichangia hoja kwenye Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, akitaka kuwaonesha Waziri wa Ujenzi na Naibu wake kwamba anachukizwa na hali ya barabara jimboni kwake kutojengwa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad