Mfanyabiashara maarufu nchini Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Capital Group Limited, Chris Kirubi, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80 familia yake imethibitisha.
Mfanyabiashara huyo mnamo Novemba 2017 alisafirishwa kwenda Marekani kwa matibabu ya miezi minne akisumbuliwa na Saratani ya utumbo.
Kwa kipindi hicho Kirubi alisema kwamba saratani aliyopata ilibainika mapema kiasi cha kuweza kutibika na kuweza kudhibitiwa