Shadrack Kapanga (34) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kuwaua Emilly Mutaboyerwa ambaye ni mama na Damita (13) na Daniela Mutaboyerwa (15) eneo la Masaki, Mtaa wa Maryknol
Kapanga ambaye ni msaidizi wa kazi za ndani alikamatwa Juni 11, 2021 eneo la Magomeni. Vitu alivyokutwa navyo wakati akitoroka ni Simu za Marehemu, Televisheni, King’amuzi cha DSTV na Rimoti
Kamanda Jumanne Muliro amesema upelelezi wa awali umebaini mtuhumiwa alifanya mauaji Juni 9, 2021 kwa kuwapiga kila mmoja kwa wakati tofauti kwa kitu kizito na kuwasababishia kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha