Mkuu wa Twitter Jack Dorsey ameweka ujumbe wenye picha ya bendera ya Nigeria mtandaoni katika hatua ambayo vyombo vya habari nchini humo vinaashiria ni kuunga mkono maandamano ya Jumamosi dhidi ya uongozi mbaya na kulalamikia kufingiwa kwa Twitter.
Ujumbe wa Bw. Dorsey umewavutia Wanageria wengi wanaotumia mtandao wa VPN kufikia programu hiyo tumishi.
Twitter inajadiliana na serikali ya baada ya kupigwa marufuku nchini humo tarehe 5 mwezi Juni.
Marufuku hiyo ilifuatia hatua ya mtandao huo kufuta ujumbe wa Rais Mohammadu Buhari lakini ofisi yake imesema hatua hiyo haihusiani kivyovyote na suala hilo.
Raia wa Nigeria siku ya Jumamosi waliandamana kulalamikia uongozi mbaya, ukosefu wa demokrasia na kupigwa marufuku kwa Twitter.
Polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanji na kuwakamata baadhi yao,kulingana na vyombo vya habari nchini humo.
Maandamano ya Jumamosi ni ya kwanza tangu maandamano ya #EndSARS ya kupinga ukatili wa polisi yaliyofanywa kwa wiki kadhaa.