Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi mkuu wa WHO, akihudhuria mkutano mjini Geneva. June 25, 2021,
Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi mkuu wa WHO, akihudhuria mkutano mjini Geneva. June 25, 2021,
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, anasema aina mpya ya virusi vya Corona iliyopewa jina la Delta imegundulika katika nchi angalau 85, na ndio aina ya virusi vinavyoambukiza kwa kasi kuliko aina zote zilizogunduliwa hadi hivi sasa.
Tedros anasema aina hiyo ya virusi vinasambaa haraka miongoni mwa watu wasiopata chanjo. Anaendelea kusema kwamba wakati baadhi ya nchi zinalegeza masharti ya afya ya umma na hatua nyingine za kijamii, tunaanza kushuhudia ongezeko la maambukizo kote duniani.
Wakati huo huo, maafisa wa afya wanasema aina mpya nyingine ya virusi kutokana na Delta, iliyogunduliwa kwanza india imejitokeza katika baadhi ya nchi ikiwemo India, Marekani na Uingereza.
Aina hii mpya imepewa jina lisilo rasmi “Delta Plus”. Maafisa wa afya wanaogopa Delta Plus inaweza kuwa na madhara zaidi kuliko Delta, ambayo pia ni aina mpya ya virusi. Wanasayansi wanaanza kufanya utafiti kuhusu aina hii mpya ya virusi hivyo.