Moto wa Alikiba Hauzimi, Naanza Kuachia Ngoma Mfululizo

 


Unaweza kusema moto wa King Kiba hauzimi hivi sasa baada ya nyota huyo wa muziki nchini kuweka wazi kuwa kuanzia sasa ataanza kuachia ngoma mfululizo bila kupumzika.

Bosi huyo wa lebo ya Kings Music baada ya kuwabariki mashabiki na ‘Ndombolo’ ameweka wazi kupitia instagram kuwa katika majira haya ya joto itakuwa ni wakati wa furaha kwani  ataachia nyimbo mfululizo mpaka pale album yake itakapotoka.

"Summer is here and it’s going to be fun , dropping music back 2 back until my album is out !!" – ameandika Alikiba.

Hivi sasa King Kiba na wasanii wake wa lebo wameachia wimbo wao mpya wa pamoja ‘Ndombolo’ ambao ni wa tatu baada ya Rhumba na Toto.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad