Mtoto anatuhumiwa kumuua Baba wa kambo





Mvulana wa miaka 17 Mombasa Kenya anatuhumiwa kwa kumuua Baba yake wa kambo kwa madai ya kwamba Baba huyo amekua akimtesa kwa kumpiga Mke wake ambae ndio Mama Mzazi wa Mtoto huyu.
Imeripotiwa kwamba siku ya tukio Marehemu alikua akigombana na Mkewe ndipo Mtoto huyo akashikwa na hasira akachukua kisu na kumchoma Baba yake mara kadhaa hadi alipofariki.

Citizen TV imeripoti kwamba Mtoto huyo ni Mwanafunzi wa kidato cha pili ambapo Shuhuda mmoja alikutana na Mtoto huyo akiwa na visu viwili na kusema ‘mimi leo nimemuweza, amezoea kumpiga Mama yangu kila siku mimi leo nimemuweza” jirani mwingine amesema “Nimeletewa kesi mara kwa mara wakiwa hawana amani Mke na Mume, nilijaribu kuwaweka pamoja lakini haikuwezekana”

Huku baadhi ya Watu mtaani wakisema Mtoto huyo amekua akivuta bangi sana na kumfanya awe mtukutu wengine wamesema alikua akifika maskani anaelezea Mama yake anavyoteswa na Baba yake vitendo ambavyo vimekua vikimuumiza.

Polisi wanamshikilia Mama wa Mtoto huyo na wanaendelea na kumtafuta Mtuhumiwa ambae alitoroka muda mfupi tu baada ya mauaji hayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad