Museveni Afuata Nyayo za Magufuli Sakata la Corona Nchini


Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewataka wananchi kutenga siku moja maalum kwa ajili ya kumuomba Mwenyezi Mungu awalinde dhidi ya janga la virusi vya corona (covid-19).

Uganda imekumbwa na wimbi la tatu la corona ambalo limesababisha Rais Museveni kuweka masharti mapya ya kujifungia na pia kusimamisha vikao vya Bunge.

Museveni aliitangaza siku ya Ijumaa, Juni 25, 2021 kuwa siku maalum ya maombi ya kitaifa, akiwataka wananchi kumlilia Mwenyezi Mungu kuhusu hali ilivyo nchini humo.

Hatua hiyo inaonesha kufuata nyayo za Hayati Dkt. John Magufuli, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye alitangaza maombi ya siku tatu ya kitaifa dhidi ya covid-19.

Hatua hiyo ilionesha kuzaa matunda, ambapo visa vya corona na hali ya ugonjwa ilionekana kupungua nchini Tanzania. Hatua hiyo ilichukuliwa kama muujiza wa aina yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu akijibu maombi ya Watanzania.

Ndugai: Kuna waliomaliza ubunge maisha yao ni magumu kweli

Katika siku tatu za hivi karibuni, Serikali ilithibitisha kuwepo kwa ongezeko la watu 126 waliopoteza maisha kutokana na corona, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa nchini Uganda.

Rais Museveni alisema kuwa idadi hiyo iliyotajwa inaweza isiwe ndio uhalisia wa hali ilivyo kwakuwa kuna baadhi ya watu wanaopata maambukizi lakini hawajarekodiwa kwenye orodha rasmi.

Inaripotiwa kuwa nchi hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa wakati wakijaribu kupambana na corona. Katika jiji la Kampala, inaonesha kuwa kuna upungufu wa vitanda vya hospitalini kwa ajili ya wagonjwa wapya, upungufu wa vifaa vya hewa ya oxygen ya kuwasaidia wagonjwa kupumua pamoja na upungufu wa vifaa vya kujikinga wakati wa kutoa huduma.

Aliyemuua George Floyd apigwa miaka 22 jela, Jaji amuongeza lingine

“Tuna ‘gloves’ chache tulizopokea kutoka NMS (Bohari ya Taifa ya Dawa) katika siku za hivi karibuni, vifaa kama vitakasa mikono na gloves tulizonazo ni chache. Pia, hata magari ya wagonjwa (ambulances) hayapo ya kutosha,” Dkt. Sam Elungat, kutoka Hospitali ya Wilaya ya Busia aliwaambia waandishi wa habari.  

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad