Mwadui FC yajigamba kuchukua point 3 mbele ya yanga kesho





FREDRIK Masombola, Kocha Msaidizi wa Mwadui FC amesema kuwa wanahitaji pointi tatu kesho mbele ya Yanga.
Mwadui FC ambayo ipo nafasi ya 18 na pointi 19 baada ya kucheza mechi 31, kesho Juni 20 ina kibarua Uwanja wa Mkapa dhidi ya Yanga.

,  Masombola amesema kuwa wachezaji wapo tayari na wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo huo.

"Timu imewasili jana na leo tumeanza mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Yanga na tunahitaji ushindi. 

"Kupoteza kwetu mechi zilizopita haina maana kwamba tutapoteza tena hapana tupo tayari na wachezaji wamepewa majukumu yao ya kufanya.

"Niwaambie mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti kwani kikubwa ni kwamba kila mchezaji anahitaji kuona tunashinda," amesema

Mchezo wao wa ligi uliopita wa ubao wa Kambarage ulisoma Mwadui 0-5 Yanga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad