Wakati joto la uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likizidi kupanda,Hawa Mniga amekuwa mwanamke wa kwanza kuchukua fomu ya urais wa shirikisho hilo.
Hawa amechukua fomu hiyo ili kupambana na rais wa TFF anayemaliza muda wake,Wallace Karia ambaye alichukua fomu ya kuwania tena nafasi hiyo Juni 8.