Ziona Chana, mwanaume ambaye alikuwa ameoa wake 39 na watoto 94 ameaga dunia nchini India.
Inaaminika kuwa baba huyo alifariki dunia Jumapili, Juni 13,2021.
Zora mwenye umri wa miaka 76 alikuwa kiongozi wa dini flani ya Kikristu ambayo inaamini katika ndoa za mitaala. Familia yake ilikuwa na jumla ya watu 167 ikiwemo wajukuu 33.
Alimuoa mke wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17 na kudai kuwa alioa wake 10 chini ya kipindi cha mwaka mmoja kulingana na Sky News.
Chana alikuwa anaishi na familia yake katika jumba la kifahari lenye ghorofa nne na vyumba 100. Jumba lake pamoja na familia yake kubwa zilikuwa zinawavutia watalii.
Dini hiyo ilianzishwa na baba yake Chana mwaka 1942 na ilikuwa inatambulika kama Chana.Waumini wa dini hiyo ni mamia ya familia kulingana na TimesLIVE.