Ndalichako: Marufuku kumfukuza mwanafunzi




Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema ni marufuku kumfukuza mwanafunzi shule wakati wa utekelezaji wa waraka wa elimu namba tatu wa mwaka 2016 unaoelezea utaratibu wa kutoa michango shuleni.


Waraka huo namba tatu wa mwaka 2016 unaainisha majukumu ya jamii na wananchi kuhusu michango.



Profesa Ndalichako alikuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Nkasi Kaskazini (Chadema) Aida Khenani ameitaka Serikali kueleza wananchi kuwa kilichobadilika ni ada tu badala ya kutamka kuwa elimu ni bure.



Pia, ametaka kujua  kuwa Serikali haioni haja ya kufanya tathimini upya ya utaratibu huo wakiwashirikisha wadau wa elimu ili kufahamu changamoto ni nini badala ya ada pekee.



Akijibu swali hilo, Profesa Ndalichako ametoa wito kwa wazazi kushirikiana na Serikali kuboresha mazingira ya shule kwasababu mazingira ya shule yanapokuwa mazuri watoto wanakuwa na uhakika wa kupata elimu bora.



“Kikubwa tunasisitiza mwanafunzi asifukuzwe shule kwababu ya michango. Katika kutekeleza waraka namba tatu wazingatie kuwa ni marufuku kumfukuza mwanafunzi yoyote kwasababu ya kukosa michango,”amesema.



Awali Naibu Waziri katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) David Silinde amesema waraka namba tano mwaka 2015 umesema kuwa elimu msingi ni bila ada.



Amesema pia, Serikali ilitoa waraka mwingine namba tatu  wa mwaka 2016 na umeainisha wajibu wa Serikali na wajibu wa mwananchi ikiwa ni pamoja kushiriki katika ujenzi wa miundombinu.



Hata hivyo, amesema wameweka fursa kuwa si wazazi wasilazimishwe kutoa michango hiyo.



 Silinde amesema wameendelea kufanyika tathimini na kwamba sasa hivi wanazaidi ya wanafunzi 14,000 ni lazima kuangalia namna gani wanasaidia elimu kwa jumla nchini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad