Ndugulile “Mtu mmoja laini moja ya simu kwa mtandao mmoja”





Serikali imesema inaandaa sheria maalumu ya mtu kuwa na laini moja ya simu kutoka kampuni moja ikiwa ni njia ya kulinda faraga za watu inayolenga kudhibiti wahalifu mtandaoni.
Katika kipindi hiki cha mpito, kampuni za mawasiliano zimetakiwa kuweka mfumo thabiti wa kuhakikisha hakuna mtu anayetoa ushirikiano kwa wahalifu.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile ameyasema hayo katika mkutano na Watendaji Wakuu wa Kampuni za Simu kujadili mambo muhimu wakati wa kuelekea awamu ya sita ya mradi wa mawasiliano maeneo ya mipakani na kanda maalumu.

“Nadhani kampuni zingine, lakini sio zote zina watu ambao sio wa kweli na wanafanya kazi na wahalifu kwa kutoa habari za siri za wateja kwa nia ovu. Hatutavumilia kuchukua hatua dhidi ya kampuni yoyote itakayotuhumiwa kuvujisha habari za wateja,” Ndugulile

Dkt. Ndugulile amesema ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia jinsi ya kutumia mfumo wa kuaminika zaidi kwa wateja kuthibitisha namba zao na kwa wale ambao hawawatambui, wanapaswa kufutiwa au kuzimwa kutoka katika mfumo.

“Hakuna haja ya kukaa na namba za watu kwa mfano mtu amesajili laini nyingi na ninyi TCRA mna nguvu na mifumo ya kutambua nani ana laini nyingi, wacha tufanye hivyo na tumalize kesi hizi,” Ndugulile


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad