Nigeria imesema inajadiliana na Twitter,baada ya kuufungia mtandao huo wa kijamii wikendi iliyopita.
Baada ya kukutana na wanadiplomasia, Waziri wa Mambo ya nje wa wa Nigeria Geoffrey Onyeama amesema serikali inafuatilia jinsi mazungumzo yanavyoendelea kabla ya kufanya maamuzi yoyote ya ziada.
Katika hatua ya hivi punde dhidi ya Twitter, mamalaka imeagiza vyombo vyote vya habari kujiondoa katika mtandao huo.
Wanadiplomasia wa Magahribi wamekosoa marufuku hiyo wakisema uhuru wa kijieleza ni sehemu muhimu ya democrasia.
Serikali ya Nigeria imechukua hatua ya kufungia mtandao huo baada ya Twitter kuondoa ujumbe wa Rais Muhammadu Buhari wa kutishia kundi linalotaka kujitenga.
BBC ilizungumza na Gbenga Sesan wa Mpango wa Paradigm, ambao unatoa fursa za kidijitali kwa vijana kote Afrika, ambaye anasema marufuku ya serikali imefeli.