Nigeria yataka wenye mitandao ya kijamii kupata vibali vya ndani






Kampuni za mitandao ya kijamii ambazo zinataka kuendesha shughuli zao nchini Nigeria sasa zitahitajika kujisajili nchini humo na kupewa leseni na tume ya utangazaji.
Waziri wa mawasiliano,Lai Mohammed, ametoa tangazo hilo kufuatia hatua ya serikali kupiga Twitter marufuki siku tano iliyopita.

Mtandao huo wa kijamii ulifuta ujumbe wa Rais Muhammadu Buhari kwa kukiuka sheria zake lakini ofisi ya rais imepinga madai kwamba marufuku hiyo ilikuwa hatua ya kilipiza kisasi.

Baadhi ya vyombo vya habari vya kibinafsi nchini Nigeria vimepuuza amri ya kufunga akaunti zao za Twitter na kuamua kufikia mtandao huo kupitia mtandao wa VPN

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad