Dar es Salaam. Joto la uteuzi wa wakuu wa wilaya na wakuru[1]genzi wa halmashauri hapa nchini limezidi kuongezeka baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuweka wazi kwamba orodha mpya itatoka hivi karibuni.
Rais Samia alifichua siri hiyo jana jijini Mwanza, wakati akizun[1]gumza na vijana na kuongeza joto la uteuzi huo ambao unasubiriwa kwa hamu baada ya kukamilisha uteuzi wa mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na maka[1]tibu tawala wa mikoa.
Tangu alipoapishwa Machi 19, Rais Samia amekuwa akiteua vion[1]gozi mbalimbali na katika teuzi hizo amekuwa akiwabadilisha vituo vya kazi wengi wao, lakini amewaondoa wachache kutokana na sababu tofauti.
Jana, Rais Samia alitengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa na Mku[1]rugenzi wa halmashauri ya Moro[1]goro, Sheilla Lukuba kwa sababu ya kutoridhishwa na walivyowaondoa wafanyabiashara wadogo (Wam[1]achinga) kwenye kituo cha mabasi cha Morogoro. Alitangaza hatua hiyo wakati akihutubia vijana wa Mkoa wa Mwanza na kueleza kitendo cha kunyanyaswa wafanyabiashara hao si cha kiungwana na hakikuba[1]liki.
Sasa unasubiriwa uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao ndio wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na wananchi huku baadhi ya maeneo wakitaka vion[1]gozi hao waondolewe na sehemu nyingine wakitaka viongozi hao waendelee kubaki.
Rais Samia anatarajiwa kuteua wakuu wa wilaya za Tanzania Bara 161 na wakurugenzi wa hal[1]mashauri 185 watakaomwakilisha katika maeneo yao na kusimamia shughuli za kila siku za utendaji wa Serikali.
Mkeka unakuja
Jana, wakati akizungumza na vijana jijini Mwanza alikofanya ziara ya siku tatu, Rais Samia alise[1]ma “Kuna mkeka wa maDC (wakuu wa wilaya) utakaotoka karibuni, nataka kuwaambia kwamba wote ni vijana. Kwa hiyo, hizo ndiyo fur[1]sa mlizonazo vijana.” Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Stephen Men[1]go aliiambia Mwananchi kuwa Rais Samia amekuwa akiwapa nafasi ya pili watendaji wake kujirekebisha na kutenda yale ambayo anataka yafanyike katika utawala wake.
“Natarajia kuona akiwabadilisha vituo vya kazi wengi wao na kuw[1]aondoa wachache ambao wame[1]onekana kuwa tatizo. Ameanza kufanya hivyo na ataendelea pia katika uteuzi huu,” alisema mwa[1]nazuoni huyo.
Hadi sasa kuna wilaya saba ambazo ziko wazi kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo uteuzi. Wilaya hizo ni Kinondoni (Dar es Salaam), Same, Rombo na Hai (Kilimanjaro), Uvinza (Kigo[1]ma), Muheza (Tanga) na Moro[1]goro.
Wilaya ya Kinondoni imebaki wazi baada ya aliyekuwa mkuu wa Wilaya hiyo, Daniel Chongolo kuteuliwa na halmashauri kuu ya Taifa ya CCM kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.
Wilaya ya Hai imebaki wazi baa[1]da ya Rais Samia kumsimamisha kazi Lengai Ole Sabaya kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka zinazomkabili na suala lake liko kortini na mikononi mwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Vilevile, Wilaya ya Same imebaki wazi baada ya Rosemary Senyam[1]ule kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwamvua Mrindiko kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Wakuu wa wilaya wengine wali[1]oteuliwa ni Athuman Kihamia ambaye alikuwa Rombo sasa anakuwa Katibu tawala wa mkoa wa Arusha. Mwingine ni Mwanai[1]sha Tumbo ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza, sasa ni kati[1]bu tawala wa mkoa wa Pwani.
Mbali na Wakuu wa Wilaya, Rais Samia anatarajiwa pia kuteua wakurugenzi wa halmashauri ambapo mabadiliko makubwa yanatarajiwa kufanyika katika eneo hilo kutokana na tuhuma za ubadhirifu, usimamizi mbovu wa miradi na matumizi mabaya ya madaraka zinazowakabili wakuru[1]genzi wengi.
Kwa sasa halmashauri saba za Morogoro, Temeke, Buhigwe, Sen[1]gerema, Sumbawanga, Nachin[1]gwea na Bahi hazina wakurugenzi baada ya kusimamishwa kazi kwa nyakati tofauti wakituhumiwa kutenda makosa mbalimbali, iki[1]wemo ubadhirifu na usimamizi usioridhisha wa miradi ya maendeleo.