R. Kelly Awatimua Wanasheria Wake




MKALI wa muziki wa RnB Duniani, R. Kelly amewatimua kazi mawakili wake wawili Steve Greenberg na Michael Leonard ikiwa ni miezi miwili kabla ya kesi  yake kusikilizwa.

 

Kupitia kikao kifupi na Mahakama mapema wiki hii R. Kelly ameeleza kuwa amewafuta kazi mawakili hao kwasababu hawakuwa vizuri kwenye suala la uwajibikaji na amepanga kuongeza timu ya wanasheria wapya ili kuziba nafasi hizo zilizoachwa wazi mapema kabla ya kesi yake.

 

Kelly amemthibitishia Jaji wa Mahakama Ann Donnelly kwamba ataendelea kufanya kazi na timu ya wanasheria wake Becker na Farinella ambao wamesalia kwenye ile timu ya watu wanne ili kushughulikia kesi yake inayomkabili ya unyanyasaji wa kingono.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad