Rais Museveni awateua wanawake 10 katika baraza lake jipya la mawaziri.Image caption: Rais Museveni awateua wanawake 10 katika baraza lake jipya la mawaziri.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amefanya uteuzi wa baraza jipya la mawaziri 31 na manaibu waziri 50.
Baraza hilo linajumuisha wanawake 10.
Jessica Alupo, ambaye ni meja mstaafu wa jeshi, ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais. Ni mwanamke wa pili katika historia ya nchi hiyo kuteuliwa katika wadhifa huo. Alupo aliwahi kuhudumu kama Waziri wa Elimu.
Robinah Nabbanja, afisa wa ngazi ya juu wa chama tawala, ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu na kiongozi wa shughuli za serikali bungeni. Alikuwa naibu waziri wa afya.
Rebecca Kadaga, wakili na mwanasiasa wa zamani ambaye hadi uteuzi wake katika baraza la mawaziri alikuwa spika wa bunge amepewa wadhifa wa naibu waziri mkuu wa kwanza. Pia amepewa jukumu kusimamia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Baraza hilo la mawaziri pia linajumuisha maafisa wapya kutoka jeshini. Kamanda Mkuu wa sasa wa Majeshi, GJenerali David Muhoozi, ndiye naibu waziri wa mambo ya ndani. Jenerali eneral Muhoozi pia anawakilisha jeshi bungeni .
Mmoja wa mawakili wa kibinafsi wa rais, Kiryowa Kiwanuka, ameteuliwa kuwa Mawanasheria Mkuu.
Sam Kuteesa, ambaye amekuwa Waziri wa Uganda wa Mambo ya nje kwa muda mrefu, ameondolewa katika baraza la mawaziri.