Samia amtumbua DC Morogoro, mkurugenzi kwa sababu ya wamachinga


 


Mwanza. Rais Samia Suluhu Hassan amewafuta kazi mkuu wa Wilaya ya Morogoro na mkurugenzi wa halmashauri hiyo baada ya kuchukizwa jinsi walivyoshughulikia suala la wafanyabiashara wadogo wilayani humo.


 Akizungumza leo Jumanne  Juni 15, 2021 katika mkutano wake na  vijana uliofanyika mkoani Mwanza, Rais Samia amemwagiza Waziri wa Tamisemi, Ummy Mwalimu  kutekeleza agizo lake la kutengua uteuzi wa viongozi hao.


"Kutokana na kutengewa eneo lililo nje lisilofikiwa na wateja, wamachinga Morogoro waliamua kurejea mjini na mamlaka ikaingilia kati kuwaondoa. Sijafurahia jinsi walivyotendewa na DC na mkurugenzi hawana kazi."


"Kwa sababu kuna njia nzuri zaidi ambayo ingetumika kushughulikia hilo..., sio ile iliyotumika. Sijafurahishwa nakuagiza Waziri wa Tamisemi shughulikia hilo," amesema Samia.


Japo majina ya viongozi waliopoteza nafasi zao hayakutajwa lakini mkuu wa Wilaya ya Morogoro ni Bakari Msulwa na mkurugenzi ni Sheila Lukuba.


Viongozi hao wanakuwa wa kwanza kupoteza nafasi zao kwa kutoshughulikia vyema suala la wamachinga tangu Rais Samia alipoingia madarakani Machi 19, 2021.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad