Samia Mbioni Kupangua Wakuu wa Wilaya

 



Mwanza.  Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema atafanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya hivi karibuni na atawapa nafasi zaidi vijana.


 Akizungumza na vijana mkoani Mwanza leo Jumanne Juni 15, 2021 kiongozi mkuu huyo wa nchi amesema kipindi hiki ni cha vijana kusimamia maendeleo ya nchi.


“Kuna mkeka wa ma Dc (wakuu wa wilaya) utakaotoka hivi karibuni..., ninataka kuwaambia  wote ni vijana. Kwa hiyo hizo ndizo fursa mlizonazo vijana ingawa baadhi yenu tunavyowapa fursa hizi mnakwenda kufanya mnayofanya na mnatuangusha,” amesema Samia.


Amewataka vijana wanaopata fursa hizo walitumikie Taifa kwa umakini na ufanisi, “Sisi viongozi wenu kazi yetu kuonesha njia vijana wapite na muendelee na safari ya maendeleo lakini pia kulilinda na kuendeleza Taifa hili.”


Amesema hata baraza la mawaziri wengi ni vijana  sambamba na wakuu wa mikoa na  makatibu tawala wengi ni vijana.


“Mfano mzuri kule Zanzibar, Rais wa Zanzibar (Dk Hussein Mwinyi) ni kijana na tulimpendekeza tukijua hii ni enzi ya vijana, kwa hiyo vijana tunaomba mjitambue kwamba nyinyi sasa ndio wenye maono ya nchi hii sasa hivi na baadaye na mwelekeo ni huo,” amesema kiongozi mkuu huyo wa nchi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad