Serikali yaliomba Bunge kufumua sheria 13

 


Dodoma. Serikali imewasilisha bungeni muswada wa mapendekezo ya marekebisho ya sheria 13 ili kuendana na mazingira ya utedaji kazi.

Miongoni mwa sheria hizo ni sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sheria ya Stahili na Mafao ya Kustaafu ya Majaji, idara ya Bohari ya Dawa, Sheria ya Madini,Sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.


uratibu wa ajira za wageni, Sheria ya mafao ya kustaafu ya viongozi wa kisiasa, Sheria ya uwazi na uwajibikaji katika rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia, Sheria ya shirika la Posta Tanzania, Sheria za huduma za mawasiliano kwa wote, Sheria ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi na sheria ya fidia kwa wafanyakazi.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi amewasilisha mapendekezo ya marekebisho ya sheria hizo akisema yanalenga kuondoa mapungufu ambao umejitokeza katika sheria hizo wakati wa utekelezaji wa baadhi ya masharti katika sheria hizo.

Profesa Kilangi amesema hatua hiyo itaongeza tija na ufanisi wa Idara mbalimbali hususan wakati huu mbapo Serikali inakusudia kuingia katika uzalishaji na uwekezaji.

Miongoni mwa marekebisho hayo ni kuweka kisheria faini zinazotozwa na mahakama na kutambua makosa ambayo hayajatajwa na sheria hii ambayo kimsingi yamebainika kuwa moja ya vyanzo vya ajali za barabarani.

Makosa hayo ni kuendesha gari huku ukiongea na simu ya kiganjani, kuendesha gari bila kufunga mkanda ambako wanalenga marekebisho yakaimarishe mfumo wa usimamizi wa sheria ili kulinda maisha ya watu na mali zao watumiapo barabara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad