Serikali Yaruhusu Usafirishaji wa Makinikia



Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imesharuhusu usafirishaji wa makinikia baada ya kuweka utaratibu mzuri wa ukusanyaji mapato.


Katika kipindi cha Maswali ya papo kwa hapo Bungeni leo, Waziri Mkuu amesema sheria imewekwa vizuri na kumekuwa na udhibiti wa kutosha ili kutokupoteza mapato.


Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Idd Kassim, mbunge wa Msalala (CCM) ambaye ametaka kujua Serikali ilizuia usafirishaji wa makinikia na nini kimesababisha kuanza tena kuyasafirisha kwenda nje ya nchi.


Waziri Mkuu amesema Serikali ilisitisha usafirishaji wa makinikia tangu 2017/18 kutokana na kubaini kulikuwa na wizi na udanganyifu.


Amesema zuio hilo lililenga kufanya uchunguzi wa kujiridhisha na kutaka ianzishwe kampuni ya wazawa ambapo ilianzisha Kampuni ya Twiga ambayo Serikali ina ubia.


Amesema kwa sasa umewekwa utaratibu mzuri wa utoaji vibali na hakuna kontena ambalo litasafirishwa kwenda bandarini bila kibali.


ADVERTISEMENT

Amesema Serikali iko makini kwa kila hali baada ya kuibiwa kwa muda mrefu katika usafirishaji huo.


Kingine amesema kulikuwa na madini zaidi ya aina moja katika mchanga unaosafirishwa lakini wahusika hawakuyasema hadi timu iliyoundwa ilipotoa taarifa yake.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad