Kutokana na style ya kuwa na swaga na kuvaa mavazi ya kiume msanii Sister P amesema baadhi ya wanaume walikuwa wanaogopa kumfuata kwa sababu walijuwa atawazingua au kuwapiga ngumi.
"Mimi ni mgumu kwa hiyo tangu zamani watu walikuwa wanaogopa kunifuata, walikuwa wananichukulia kama muhuni mwenzao, nahisi walikuwa wanajua wakinifuata naweza nikawapiga hata ngumi"
Pia ameongeza kusema "Watu wananishangaa ninavyovaa ila nina bahati hata wapenzi wengi ambao huwa nawapata huwa wanataka nibaki hivi, lakini sasa hivi hata watu niliokuwa nawaheshimu wananitongoza kitu ambacho sikipendi".