Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ jumapili hii inajitupa uwanja wa hayati Benjamin Mkapa jijini Dar-es-Salaam kuwakabili Malawi The flames saa 10:00 jioni ikiwa ni mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwenye kalenda ya FIFA.
Katika mchezo wa leo, Taifa Stars itawakosa nyota wake wawili kwa sababu tofautitofauti miongoni mwao ambaye ni Simon Msuva anayecheza nchini Wydad Casablanca ya Morocco pamoja na nahodha Mbwana Samatta anayechezea Fenerbahce nchini Uturuki
Kwa mujibu wa meneja wa timu hiyo , mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars Nadir Haroub Canavaro amesema ‘’ kambi ipo salama wachezaji wote wapo vizuri kuwakabili wageni ,tunawakosa Samatta na Msuva tu lakini hakuna mashaka yeyote’’
‘’Ushindani wa kugombea namba ni mkubwa kila mchezaji anafanya bidii kushawishi kocha kupata nafasi ya kupangwa’’aliongeza Canavaro
Mchezo wa leo ni wa kalenda ya FIFA ambao unatumika kupanga viwango vya ubora duniani,kwa sasa Malawi ni ya 115 huku Tanzania ikiwa 137,takwimu zinaonesha wamekutana mara 7 kwa miaka ya karibuni Stars wameshinda mara 3 na Malawi mara 1 huku wakitoa sare 3