Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 28, ameieleza Crystal Palace kwamba anataka kuondoka kabla ya msimu wa mazoezi kuanza. (Times)
Kocha mpya wa Real Madrid Carlo Ancelotti yuko tayari kumtafuta aliyekuwa mshambuliaji wa iliyokuwa klabu yake Everton raia wa Brazil Richarlison, 24. (Football Insider)
Everton iko tayari kutoa ofa ya mkataba wa miaka mitatu kwa aliyekuwa kocha wa Wolves Nuno Espirito Santo, 47. (Nicolo Schira via Star)
Arsenal na Aston Villa wametenga rasmi vitita vyao kwa winga wa Argentina anayechezea Norwich anayesemekana kwamba thamani yake ni pauni milioni 40 Emi Buendia, 24. (Sun)
Barcelona inasemekana kuwa tayari kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania Ilaix Moriba, 18, licha ya timu za Manchester United, Manchester City na Chelsea kuonesha nia ya kumsaka. (Mail)
Liverpool inaongoza katika mbio za kumsajili winga Raphinha kutoka Leeds lakini Manchester United na Manchester City pia nazo zina msaka mchezaji huyo Mbrazil, 24. (Gianluigi Longari via Express)
Arsenal iko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Matteo Guendouzi, 22, kwa euro milioni 10 sawa na (£8.6m) pekee. (Le10Sport via Calciomercato)
Ajax imeipiku Manchester United katika kumsajili winga wa Ghana Kamaldeen Sulemana, 19, kutoka FC Nordsjaelland. (Football Insider)
Olivier Giroud, 34, yuko tayari kuichagua AC Milan mkataba wa mshambuliaji huyo wa Chelsea raia wa Ufaransa utakapokamilika. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Sead Kolasinac, 27, kutoka Bosnia yuko tayari kuuzwa na Arsenal baada ya Schalke kusema haikuweza kubadilisha mkataba wa mkopo wa beki huyo wa kushota kuwa wa kudumu msimu huu. (Football London)
Atletico Madrid iko tayari kutoa ofa kwa kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 26, ambaye awali aliwahi kuhusishwa na Manchester United. (Marca - in Spanish)
Fiorentina ina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 26, kwa mkopo kutoka Chelsea msimu huu. (Fabrizio Romano, Twitter)
Kocha anayerejea Massimiliano Allegri alikutana na wafanyakazi wa Juventus Alhamisi, huku hatma ya mshambuliaji raia wa Ureno Cristiano Ronaldo, 36, ikiwa kipaumbele katika orodha ya ajenda zake. (Goal)
Tottenham bado inafanya mazungumzo na mshambuliaji wa Korea Kusini Heung-min Son, 28, kuhusu mkataba wake mpya na ina imani ya kufikiwa kwa makubaliano punde tu kocha wao mpya atakapochaguliwa. (Fabrizio Romano, Twitter)
Douglas Luiz anatarajiwa kusalia na Aston Villa kwasababu Manchester City haina uwezekano mkubwa wa kuzingatia kipengele cha kumnunua tena kiungo huyo wa kati Mbrazil, 23. (Express & Star)
Kocha wa Atletico Madrid raia wa Argentina Diego Simeone, 51, anakaribia kukubali kuongezwa mkataba wa miaka miwili hadi mwaka 2024. (Cadena Cope via Mundo Deportivo)
Mabingwa Ufaransa Lille inataka kumtaja Patrick Vieira, 44, kama mrithi wa aliyekuwa kocha wa timu timu hiyo Christophe Galtier. (L'Equipe - in French)
Aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal Nicklas Bendtner anapanga kuendeleza shughuli zake za kuwa kocha baada ya kutangaza kustaafu akiwa na umri wa miaka 33, ikiwa ni miezi 17 baada ya raia huyo wa Denmark kuchezea FC Copenhagen mechi yake ya mwisho. (Ekstra Bladet - in Danish)