Mwimbaji/Mwigizaji wa Marekani mzaliwa wa Harlem, New York Teyana Taylor mwenye umri wa miaka 30 amekua Mwanamke mweusi wa kwanza kutajwa na Jarida la Maxim kama Mwanamke mwenye mvuto zaidi anayeishi.
Maxim ni Jarida la kimataifa la Wanaume ambalo lililoanzishwa Uingereza mwaka 1995 na kuweka makao yake New York Marekani toka mwaka 1997, mpaka sasa ni Jarida ambalo lina Wasomaji wapatao milioni tisa kila mwezi