KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba SC na Yanga utakaochezwa Julai 3, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imewashusha pumzi mashabiki na wadau wa mpira wa miguu nchini juu ya namna ya kupata fursa ya mara nyingine kuingia katika mchezo huo.
DERBY PIC

Awali mchezo huo ambao ni kiporo ulitakiwa kuchezwa Mei 8 lakini ukasogezwa mbele baada ya kutokea sintofahamu na mchezo kuhailishwa.
Lakini leo taarifa ya TPLB imeeleza tiketi za mchezo huo zitakazouzwa ni13, 782 tu na sio vinginevyo.
Taarifa hiyo imesema kuwa mashabiki ambao walikata tiketi kwa ajili ya mchezo uliuoahirishwa Mei 08watatumia kadi zao za NCARD kuingia uwanjani.
“Hatua hiyo imekuja baada ya maamuzi yaliyofanywa awali kuhusu mashabiki ambao walikata tiketi kwa ajili ya mchezo ambao uliahirishwa Mei 8, 2021 (Simba SC dhidi ya Young Africans SC), kuruhusiwa kutumia kadi zao (NCARD) kuingia uwanjani bila kulazimika kulipia tena tiketi kwa ajili ya mchezo huo” imesema taarifa ya Bodi ya Ligi
Katika tiketi 13,782 zitakazouzwa, tiketi 2,218 ni za jukwaa la kijani (mzunguko), tiketi 11,280 ni za jukwaa la machungwa (Orange) na tiketi 284 za VIP B.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa hakutokuwa na tiketi za VIP A na VIP C zitakazouzwa kwa ajili ya mchezo huo.
Taarifa hiyo imebainisha gharama za tiketi zitakazouzwa ni kama ifuatavyo;
Mzunguko – Tsh. 7,000
Machungwa – Tsh. 10,000