RASMI sasa, Tanzania itapeleka timu nne kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika (CAF) na kombe la shirikisho kwa msimu wa 2021-2021.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 21, na Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo, timu mbili zitacheza Ligi ya Mabingwa na mbili zitacheza kombe za Shirikisho Afrika.
Taarifa hiyo imeeleza, hatua ya raundi ya awali itachezwa kati ya Septemba 17-19, 2021 huku hatua ya makundi ikitarajiwa kuchezwa kati ya Februari 11-13, 2022.
Nafasi hizo zimepatikana baada ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zilizokusanya alama nyingi zaidi kwenye viwango vya CAF.