Tshishimbi aomba kurundi ndani ya kikosi cha Yanga






IMEELEZWA kuwa nahodha wa zamani wa kikosi cha Yanga, Papy Tshishimbi ameomba kurundi ndani ya kikosi hicho ili kukitumikia kwa ajili ya msimu ujao.
Nyota huyo zama za Mwinyi Zahera alikuwa nahodha na alichimba msimu uliopita baada ya dili lake kuisha na mabosi wa Yanga kugoma kumuongezea dili jipya.

Kwa sasa yupo zake nchini Congo akikipiga ndani ya Klabu ya AS Vita ambapo alisaini dili la mwaka mmoja.

Habari zimeeleza kuwa nyota huyo ameomba kurudi Yanga kwa kuwa anaamini bado anauwezo wa kufanya vizuri.

"Tshishimbi ameomba kurudi Yanga kwa kuwa anaamini kwamba anaweza kufanya vizuri," ilieleza taarifa hiyo.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa suala la usajili kwao kwa sasa bado.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad