SOSHOLAITI ambaye ni dada wa msanii mkubwa wa Bongo Fleva ndani na nje ya Tanzania, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Khan au Esma Platnumz ameweka mambo hadharani juu ya ubuyu kwamba anatoka kimapenzi na aliyekuwa mume wa msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Ashraf Uchebe.
Gazeti la IJUMAA limemuweka mtukati Esma baada ya kuwepo kwa tetesi kwamba anapika na kupakua na Uchebe.
Katika mahojiano maalum, Esma anasema kuwa, wanaosema hayo wamefanya yote, lakini kuhusu kutoka kimapenzi na Uchebe wanamkosea kwa sababu Uchebe ni kama mtu wao wa karibu kwenye familia yao.
Esma anasema kuwa, kubwa zaidi, yeye na Shilole ni watu wa karibu mno.
“Kwa kweli nawashangaa sana watu wanaosema hivyo, kwamba nina uhusiano wa kimapenzi na Uchebe, lakini wangejua ukweli wa mambo, mimi Uchebe ni washkaji mno, kwanza sithubutu hata kidogo kufanya chochote na yeye maana ni kama kaka yangu, hebu waniache na mambo yangu mengi ya kufuatilia,” anasema Esma ambaye ni mjasiriamali wa vitambaa.
Akiendelea kuzungumza, Esma alisema anajua mambo mengi ya Uchebe na kwamba wao ni watu ambao kila mtu anajua mambo yake, sasa iweje tena wawe wapenzi kama wanavyosema, kitu ambacho kinamchefua mno.
“Nachefuka sana kwa hayo mambo yanaondelea, bora hata wangeniambia kitu kingine chochote na siyo hivyo, hebu waniache,” anasema.
Kwa upande wa Uchebe alisema kuwa, yeye anawashangaa wanaomzushia huo ujinga, sijui wanapata faida gani maana Esma ni kama dada yake tu na pia anamuheshimu mno Mama Dangote ambaye ni mama mzazi wa Esma.
“Yaani watu ukiwa karibu na mtu, basi ni tatizo kubwa, kwa hiyo wanataka nijifungie ndani kwa sababu gani? Wanipumzishe, mpenzi wangu watamuona,” anasema Uchebe ambaye aliachana na Shilole mwaka jana.
Stori: IMELDA MTEMA, DAR