Wakati Joto la Uchaguzi wa TFF likiendelea kupamba moto, Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka Nchini TFF imepitisha majina matatu kwenye nafasi ya Urais katika mchujo wa awali kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 7 mwaka huu Jijini Tanga.
Katika taarifa ambayo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Wakili Benjamin Kalume majina yaliyopitishwa katika nafasi ya Urais ni Hawa Mniga,Evans Mageuka na Wallace Karia huku Ally Mayai,Oscar Oscar na Ally Saleh wameenguliwa kutokana na kutokidhi vigezo vya kanuni za uchaguzi.
''kwa kuwa wanasimamia haki na katiba ya TFF hivyo kwa sasa ni jukumu lao kubandika majina ya wagombea wote ili kujua waliopita kwenye mchujo wa awali huku akiongezea kuwa ni ruksa kwa wagombea kuleta pingamizi lakini mapingamizi yao yawe na mashiko'
Benjamin Kalume makamu mwenyekiti wa uchaguzi amesema
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Agosti 7, mwaka huu jijini Tanga ambapo mbali na nafasi moja ya urais, kuna nafasi sita za wajumbe wa kamati ya utendaji zitagombewa.