NYOTA wanne wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 wameweka rekodi yao kwa kuhusika kwenye mabao mengi kuliko wachezaji wengine wote Bongo.
Kwa upande wa washambuliaji ni John Bocco ana mabao 13 na pasi tatu za mabao, Meddie Kagere ana mabao 11, Chris Mugalu ana mabao 10 na pasi mbili za mabao huku kinara wa pasi za mwisho Clatous Chama akiwa na mabao 7 na pasi 13 za mabao.
Jumla nyota hawa wamehusika kwenye mabao 59 ambayo haijafikiwa na timu yoyote hata zile zilizo ndani ya tatu bora jambo ambalo ni rekodi kwa msimu huu ambao umekuwa na ushindani mkubwa.
Ikiwa na pointi zake 67 ipo nafasi ya kwanza na imefunga jumla ya mabao 64 nafasi ya pili ipo mikononi mwa watani zao wa jadi ambao ni Yanga wana pointi 61 na wamefunga jumla ya mabao 43.
Kwa upande wa Azam FC inayonolewa na George Lwandamina safu yao ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 44 na ina pointi 60.
Ni Coastal Union inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda rekodi zinaonyesha kwamba safu yao ya ushambuliaji imefunga mabao machache ambayo ni 19 katika mechi 29 ipo nafasi ya 14 na ina pointi 33.
Gomes aliliambia Championi Jumamosi kuwa kikubwa ambacho amewaambia wachezaji wake ni kutumia nafasi zote ambazo wanazipata ndani ya uwanja ili kuweza kushinda mechi zao