WEMA Sepetu @wemasepetu amefilisika au kuna jambo nyuma ya waganga wa kienyeji ambao ameamua kuwatangazia huduma zao kwenye kurasa zake za Instagram?
Kitendo hicho ni kama kimemponza Wema, baada ya baadhi ya watu kuonesha masikitiko yao kwa mlimbwende huyo kujihusisha na matangazo hayo ambao malipo yake ni kiduchu.
“Yaani Wema amefikia maisha ya kubangaiza shilingi elfu 20 kwa waganga wa kienyeji, inasikitisha,” aliandika mtu mmoja kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Mbali na kufuria wanakomhusisha nako wengine wamekwenda mbali kwa kuwaponda baadhi ya wanganga wa kienyeji kuwa huduma zao nyingi zimejaa harufu ya utapeli na kumuonya Wema asije kujikuta katika mtego wa utapeli.
Kwa mujibu wa tangazo la mganga mmoja kwenye ukurasa wa Wema linasema mganga huyo anatoa dawa ya mvuto mapenzi, kumvuta aliye mbali, kutoa utajiri, kumchochea mpenzi akupe unachotaka na kumfunga mpenzi wako asiwe na mpenzi mwingine.
Baadhi ya watu wanasema Wema anajidhalilisha na hivyo kumtaka aachane na matangazo hayo ya wanganga wa kienyeji. Wewe unamshauri nini Wema?