Watu wawili wakamatwa wakiwa utupu,watozwa faini kukiuka masharti ya covid




Watu wawili waliokuwa wakiota jua nchini Australia wametozwa faini kwa kukiuka masharti ya kupambana na Covid baada ya kukurupushwa na mnyama aina ya paa hali iliyowafanya kuokolewa kwenye eneo la kichakani.
Wanaume hao waliokuwa wakiota jua ufukweni kusini mwa Sydney,walipatikana baada ya kuomba msaada.

Walitozwa faini kiasi cha pauni 547 kwa kuvunja masharti ya wataalamu wa afya waioweka marufuku watu walio mjini Sydney kusafiri nje ya eneo hilo.

Mji huo uko kwenye marufuku ya kutotoka nje ukipambana na kirusi cha corona cha Delta.

Kamishna wa polisi Mick Fuller alizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo Jumatatu.

''Ni wazi kuwaweka watu hatarini kwa kuondoka nyumbani bila sababu inayofaa, na nadhani zaidi ya hayo, kupotea katika bustani ya kitaifa na kugeuza rasilimali muhimu mbali na operesheni ya afya, nadhani wanapaswa kuwa na aibu."

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, mamlaka zilimpata mwanaume wa miaka 30 akiwa utupu kwenye hifadhi ya taifa ya Royal kijiji cha Otford , na baada ya upekuzi, kwa usaidizi wa helikopta, na kumpata mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 49, ambaye alikuwa hajavaa nguo vizuri.

Wanaume hao waliwaambia maafisa kuwa walikuwa kwenye ufukwe ulio eneo la karibu waliposhtuliwa na mnyama paa na kukimbilia vichakani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad