Yanga yasaka beki na kiungo kutoka DR Congo





IMEELEZWA kuwa nyota wawili wa Yanga ambao wanatoka DR Congo, Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe wamefanikisha usajili wa beki wa AS Vita, Shaaban Djuma pamoja na kiungo ambaye anawindwa na Yanga.

Habari zinaeleza kuwa bosi wa Yanga, Injinia Hersi Said kutoka wadhamini wa Yanga, GSM akiwa ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Usajili ndani ya kikosi cha Yanga kwa sasa yupo zake Congo kwa ajili ya kukamilisha madili ya nyota wawili watakaoibuka ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.

Miongoni mwa nyota ambao wanahitajika ni pamoja na Djuma ambaye ni beki huku jina la kiungo mmoja likiwekwa kapuni ila naye ni kutoka Congo.

Kuhusu Djuma habari zinaeleza kwamba mkataba wake utakapomalizika ndani ya AS Vita atajiunga na Yanga hivyo Injinia amekwenda kumaliza mchezo mazima.

Taarifa zimeeleza kuwa ambao wamerahisisha kazi na kufanya jambo hilo kufanikiwa ni nyota Tonombe na Kisinda ambao ndio walitumia nguvu nyingi kuwashawishi nyota hao kuibukia Yanga.

Nyota hao wawili wanatarajiwa kujiunga na Yanga, Julai kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22.

"Kwa sasa maandalizi ya msimu ujao yameanza na ikumbukwe kwamba Djuma awali Simba walikuwa wanamhitaji hivyo wasahau kwa sasa na kuna kiungo mwingine huyu jina lake ni siri maana wakijua basi itakuwa vurugu," ilieleza taarifa hiyo.

Mshauri wa Yanga, raia wa Afrika Kusini, Senzo Mazingisa, hivi karibuni alisema: “Tayari tumekamilisha usajili wa baadhi ya wachezaji na katika hili la usajili, tumekuwa tukifanya kwa usiri mkubwa.

“Kikubwa hatutaki kuingiliana katika usajili na timu pinzani kwa kuhakikisha tunawasajili wachezaji wote walio kwenye mipango yetu," 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad